Ikiwa leo ni siku ya Afya ya akili Duniani inayoadhimishwa Oktoba 10 ya
kila mwaka, wagonjwa wenye matatizo hayo yaliyosababishwa na Matatizo
mbalimbali wameitaka serikali na jamii kuwathamini wauguzi na madaktari
wanaowahudumia
Nchi yetu ina zaidi ya watu 450,000 wenye matatizo ya afya ya akili ambao wengi wao ni
vijana wenye umri wa kuanzia miaka 15 na kuendelea tatizo lililotajwa
kusababishwa na matumizi ya madawa ya kulevya ikiwemo uvutaji wa bangi.
Waziri
wa afya na ustawi wa jamii Tanzania Dkt. Seif rashid ametoa takwimu hizo leo
kupitia tovuti yao ya afya kuelekea maadhimisho ya siku ya Afya ya akili
duniani ambayo kitaifa yataadhimishwa hii leo tarehe 10 mwezi huu katika
viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam.
Dkt.
Seif amesema ugonjwa wa afya ya akili
umekuwa ukiwakumba wazee ambapo umekuwa ukiathiri uwezo wa mtu kufikiri,
kuhisi, kutambua na kutenda na hivyo kuwa na mwenendo au tabia tofauti
usioendana na jamii na kushauri kufikishwa katika vituo vya afya au
hospitali kwa mtu mwenye dalili kama hizo.
MAONI YANGU
Kuna uhaba mkubwa wa hospitali na vituo
vya kutibu maradhi ya akili nchini na hata hivyo vichache vilivyopo havina
watoa huduma wa kutosha. Kwa mfano hospitali ya rufaa ya magonjwa ya akili ya
Mirembe ina daktari bingwa mmoja huku ikiwa na upungufu wa madaktari 150. Ni
wazi kwa kuangalia hospitali hii kubwa hali itakuwa mbaya zaidi katika
hospitali za mikoa na wilaya.
Sambamba
na
hilo pia jamii inagubikwa na unyanyapaa kwa wagonjwa wa akili huku
mateso na
manyanyaso kwa wenzetu hawa yakionekana kama kitu cha kawaida katika
jamii.
Kuna taarifa nyingi za kubakwa na kunyanyaswa kijinsia wanawake wenye
matatizo
ya akili huku jamii ikilifumbia macho suala hili.Hivyo ni wajibu wa
wadau wa sekta ya afya kuanzia serikali na watu binafsi kuona uzito wa
jambo hili na kulipatia ufumbuzi
No comments:
Post a Comment