Matokeo ya timu ya Arsenal kushinda 2-1 dhidi ya Anderlecht kwenye ligi ya mabingwa ulaya juzi jumatano yameifanya furaha ya meneja na kocha klabu hiyo Arsene Wenger kusherekea siku yake.
Kieran Gibbs akishagilia bao la kwanza |
Kocha huyo katika mechi ya juzi ametimiza miaka 65 ya kuzaliwa kwake huku akiwa tayari ametimiza miaka 18 ya kuifundisha timu hiyo,katika mechi 1000 akiwa na washika bunduki hao ni mechi 600 tu ndizo alizofanikiwa kushinda.
Katika mechi ya juzi furaha ya wenger ingekuwa matatani kutokana na timu yake kutangulia kufungwa 1-0 ktk dakika ya 71 bao ambalo lilifungwa kwa kichwa na Andy Najar wa Anderlecht.Katika dakika ya 88 Kieran Gibbs aliisawazishia timu yake na kisha Podolski aliyetokea benchi kuchukua nafasi ya Jack Wilshere alifanikiwa kupachika bao la ushindi katika dakika za majeruhi na kumfanya Wenger kuruka kwa furaha.
Lukas Podolski akifurahia bao la ushindi |
No comments:
Post a Comment